Chuji atia neno ishu ya Ngoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Feb 2018
Chuji atia neno ishu ya Ngoma
Kiungo wa zamani wa Yanga Athumani Iddi Chuji ametoa maoni yake juu ya sakata la mshambuliaji raia wa Zimbabwe Donald Ngoma ambaye ni majeruhi.

Akihojiwa katika kipindi cha Spoti Hausi kinachorushwa na Global TV Online jana, Chuji amesema kama angekuwa kiongozi wa Yanga tayari angekuwa amemuonyesha Ngoma mlango wa kutokea.

Chuji amesema kuendelea 'kumbembeleza' mchezaji huyo ni kuzidi kushusha morali ya wachezaji wengine ambao wanaitumikia Yanga kwa 'jasho na damu'.

"Niseme kuwa, siku zote ili ushindi upatikane ni lazima uwepo umoja na ushirikiano na kila mmoja kutimiza majukumu yake ya ndani ya uwanja katika kuhakikisha kila kitu kinafanikiwa.

"Kiukweli, mimi kama ningekuwa kiongozi wa Yanga nikuhakikishie huyo Ngoma nisingeweza kumvumilia ningemtimua, yaani ni bora tukabaki wachache katika timu tungepambana wenyewe kuliko kubaki na mchezaji anayeturudisha nyuma.

"Angeondoka yeye, angekuja mchezaji mwingine mwenye uwezo mkubwa, wapo wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa zaidi ya huyo Ngoma wanayemnyenyekea,Ò€ alifunguka Chuji.

Kumekuwa na sintofahamu juu ya hatma ya mshambuliaji huyo ambaye taarifa zake zimekuwa na mkanganyiko mkubwa.

Baada ya kuibuliwa tetesi kuwa uongozi ulikuwa mbioni kumuondoa kikosini, tayari taarifa hiyo imekanushwa na inadaiwa kuwa Ngoma ataanza mazoezi karibuni kwa kuwa ameshapona majeraha yake.

Ngoma ni mchezaji mzuri, iwapo taarifa ya kurejea kikosini kuanza mazoezi ikiwa ni ya kweli ataongeza nguvu katika kikosi cha Yanga ambacho sasa kinamtegemea Obrey Chirwa katika kuzifumania nyavu.

Muhimu ni uongozi wa Yanga kumaliza sintofahamu hiyo mapema ili kutuliza 'mzuka' wa WanaYanga ambao wanaonekana kuchoshwa na 'sarakasi' zinazofanywa na uongozi juu ya mchezaji huyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
10h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’