Jumapili pale uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga itakuwa uwanjani kuwakabili watani zao Simba kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC
Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kuangukia katika kombe la Shirikisho, huu ni mchezo muhimu kwa Yanga kuwafuta machozi mashabiki wake
Wachezaji wa Yanga wanafahamu ni kwa kiasi gani mashabiki wao wameumizwa na matokeo ya ligi ya mabingwa, wanafahamu kupitia mchezo huu watarejesha morali ya timu kuelekea mchezo wa Shirikisho dhidi ya Club Africain ambao utapigwa Novemba 02
Viingilio vya mchezo huo vimetangazwa mapema, ni muhimu kuhakikisha umekamata tiketi yako ili kuepuka changamoto za kununua tiketi mwishoni




ADVERTISE HERE