Vijana wetu Serengeti Girls U17 wameandika historia huko India wakifanikiwa kutinga robo fainali michuano ya kombe la Dunia
Leo Serengeti Girls wametoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Canada na hivyo kumaliza katika nafasi ya pili kundi D wakifuzu pamoja Japan ambao ni vinara wa kundi hilo baada ya kushinda mechi zote tatu
Serengeti Girls ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Japan, wakashinda 2-1 dhidi ya Ufaransa
Kwa hakika Tanzania imeandika historia huko India, mara ya kwanza kushiriki na wamefanikiwa kutinga robo fainali...!
ADVERTISE HERE