Mafanikio katika soka hupimwa kwa idadi ya makombe

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
19 Oct 2022
Mafanikio katika soka hupimwa kwa idadi ya makombe

Basi utasikia sisi tumeingia makundi wao wanahangaika tu. Ooh.. mara Yanga timu mbovu kazi yao kukamia ligi ya ndani tu wakienda Kimataifa hawana lolote

Katika michuano yoyote, mwishoni kunakuwa na zawadi kubwa ya mshindi ambayo ni kombe ikiambatana na zawadi nyingine

Tangu msimu uliopita Yanga imekusanya jumla ya mataji manne, ligi kuu, kombe la FA na Ngao ya Jamii mara mbili

Yanga ndio klabu iliyopata mafanikio zaidi hapa Tanzania katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021,

Lengo kuu la Yanga katika kushiriki michuano mbalimbali ni kushindana na kushinda

Ni sahihi mashabiki wa Yanga kukasirishwa na matokeo ya kule Sudan kwa sababu dhamira ilikuwa kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

Hata hivyo Wananchi wana nafasi nyingine ya kupambana kwenye michuano ya kombe la Shirikisho kutimiza mipango yao

Unajua kushiriki michuano ya Kimataifa na kuondoshwa pasipo kuchukua ubingwa hakukupi sifa yoyote. Anayesifiwa ni bingwa tu, wengine watapewa pongezi za faraja

Mafanikio ya timu katika michuano mbalimbali yanapimwa kwa idadi ya makombe ambayo timu imechukua katika michuano hiyo

Hakuna kombe linaitwa raundi ya kwanza, makundi, robo fainali au hata nusu fainali

Kama unataka upewe heshima unapaswa kuwa bingwa sio kutamba nimetolewa katika hatua fulani, hiyo sio sifa!

Ni bahati mbaya soka letu limetawaliwa na propaganda zaidi ndio maana kuna timu zinaajiri watu maalum kwa ajili ya kufanya propaganda

Hiki kinakuwa kichaka cha wajanja wachache walio kwenye uongozi kujificha pale mambo yanapokuwa mabaya

Sasa hivi kuna timu hapa Tanzania ikifika robo fainali katika michuano fulani viongozi na wawekezaji wake wanapongezwa na mashabiki kutembea mitaani vifua mbele eti wametolewa robo fainali!

Mimi sijawahi kusikia ubingwa wa robo fainali, au kuna yeyote aliyewahi kusikia timu imepewa kombe kwa kufika robo fainali au makundi?

Jambo la msingi hapa ni kuwa Wanayanga hampaswi kukata tamaa eti kwa kuwa timu yenu imetolewa hatua ya makundi ligi ya mabingwa, wakati mna uhakika msimu huu timu yenu haikuwa tayari kuwa bingwa wa michuano hiyo

Muhimu ni kujipanga ili kuhakikisha timu inafanya vyema kwenye kombe la Shirikisho na lengo la huko iwe ni kuchukua ubingwa na sio kufika robo fainali au makundi kama wale wengine kwani hakuna kombe la robo fainali au makundi

Huu unyonge tunaojivika wakati mwingine hupelekea kutofanya vizuri katika mashindano makubwa tunayoshiriki

Lengu kuu katika mashindano yote iwe ni kutwaa ubingwa halafu mwisho wa msimu tutahesabu nani amefanikiwa zaidi kwa kuangalia idadi ya makombe aliyochukua

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’