Droo ya mtoano kombe la Shirikisho barani Afrika imefanyika leo nchini Misri ambapo Yanga imepangwa kucheza na Club Africaine ya Tunisia
Mchezo wa kwanza utapigwa Novemba 02 uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na mchezo wa marudiano kupigwa Tunisia wiki moja baadae
Club Africane waliwaondoa Kipanga Fc kwa kuwachapa mabao 7-0
Mchezo wa kwanza uliopigwa visiwani Zanzibar ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana na Club Africane kushinda 7-0 kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa Tunisia
ADVERTISE HERE