Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said ameahidi kuwaongezea bonus wachezaji iwapo leo watafanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Majira ya saa tatu usiku Yanga itashuka uwanja wa Al Hilal kuwakabili wenyeji wao Al Hilal katika mchezo muhimu wa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo au hata kupata matokeo ya sare ya zaidi ya bao moja ili kuweza kutinga makundi
Ni utamaduni wa Yanga kuwapa wachezaji bonus kila wanaposhinda mechi katika michuano mbalimbali wanayoshiriki lakini kutokana na umuhimu wa mchezo wa leo, bonus yake itakuwa tofauti
"Hatuna cha kupoteza hapa Sudan. Tunataka kufuzu kwenda hatua ya makundi. Huu ni mchezo muhimu sana kwetu msimu huu na nimeandaa 'bonus' nyingine maalum ili muone umuhimu wa sisi kufuzu. Nendeni mkapambane kutengeneza historia ya klabu yetu," alisema Hersi wakati akizungumza na wachezaji wa Yanga kuelekea mchezo huo
Katika hatua nyingine, wanafunzi Watanzania wanaosoma nchini Sudan watakuwepo uwanja wa A Hilal kuwapa hamasa wachezaji wa Yanga katika mchezo huo
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amefanya jitihada kuhakikisha wanafunzi hao wanafika kuwaongezea nguvu wachezaji katika mchezo huo muhimu