Saa chache zimesalia kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa huko Sudan kuanzia saa tatu usiku
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo au kupata sare ya kuanzia mabao mawili ili kujihakikishia tiketi ya kucheza hatua ya makundi
Kikosi cha kocha Nasreddine Nabi kilitua Sudan jana mchana ambapo usiku wachezaji wakapata nafasi ya kufanya mazoezi kunako dimba la Al Hilal
Nabi aliweka bayana kuwa dhamira ya timu yake ni kushinda mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali
Aidha, Nabi alidokeza kuwa kikosi kitakachoshuka dimbani leo kitakuwa na mabadiliko kidogo tofauti na kile kilichocheza mchezo wa kwanza uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 jijini Dar es salaam
Nabi anafahamu mazingira ya Sudan, amewahi kuinoa klabu ya Al Hilal, jana Al Hilal walimzawadia jezi katika kutambua mchango wake katika timu hiyo

Utakuwa mchezo mgumu lakini Wananchi wana imani kubwa kwa Nabi na kikosi chake katika kuipigania nembo ya Yanga siku ya leo
Nabi amewasoma Al Hilal katika mchezo uliopita, mabadiliko ya kikosi leo yatakuwa karata muhimu ambayo huenda ikaipa Yanga ushindi