Mshambuliaji kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga Fitson Mayele amesema wachezaji wako tayari kwa majukumu yaliyopo mbele yao huko Sudan
Yanga iliondoka jijini Dar es salaam Alfajiri ya leo Jumaosi kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Hilal
Mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 hivyo kuilazimu Yanga kusaka ushindi ugenini ili iweze kufuzu hatua ya makundi
Mayele amefichua ahadi aliyompa kocha wake wa zamani Florent Ibenge ambaye sasa anainoa Al Hilal
"Kabla ya mchezo wa kwanza dhidi ya Al Hilal, nilimpigia simu kocha Ibenge na kumwambia akija Tanzania nitafunga na pia nikienda Sudan nitafunga tena," alisema Mayele
Mayele alifunga bao pekee la Yanga katkika mchezo uliopigwa jijini Dar es salaam na atahitaji kutimiza ahadi yake kwa kufunga tena huko Sudan