Yanga yajifua kuiwinda St Louis

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Feb 2018
Yanga yajifua kuiwinda St Louis
Kikosi cha Yanga kesho kinaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam baada ya mapumziko ya siku moja.

Jana Yanga iliifumua Majimaji FC mabao 4-1 kwenye uwanja wa Taifa na kama ilivyo kawaida wachezaji walipewa mapumziko siku ya leo.

Yanga inajiandaa na mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya St Louis.

Mchezo huo utapigwa Jumatano ijayo February 21, visiwa vya Shelisheli ambapo Yanga tayari iko mbele kwa bao 1-0.

Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa wachezaji wannne wataendelea kukosekana kikosini kutoka na majeruhi.

Wachezaji hao ni Amissi Tambwe, Abdallah Shaibu, Yohana Nkomola na Donald Ngoma.

Kiungo Thabani Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji watakaokuwemo kwenye kikosi cha Yanga kitakachojifua uwanja wa Polisi kesho.

Yanga inatarajiwa kuondoka Jumapili kwenda Shelisheli
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’