Viongozi wa Yanga wametumia 'akili nyingi' kutegua mtego ambao ungeweza kuwanasa kule Sudan kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa siku ya Jumapili
Msafara wa watu 51 unaojumuisha wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki walifanya vipimo vya covid siku chache zilizopita ambapo majibu yanatarajiwa kutolewa leo
Majibu ya vipimo hivyo yatakuwa halali ndani ya saa 72 na hivyo Yanga itayatumia kule Sudan kwa maana hawatafanya tena vipimo nchini humo
Yanga itaondoka Sudan baada ya mchezo wakiwa ndani ya saa 72 na hivyo kuepuka kabisa kufanya vipimo vya covid nchini Sudan
Ikumbukwe baada ya mchezo dhidi ya Al Hilal, wiki ijayo Yanga itamenyana na watani zao Simba katika mchezo wa ligi kuu
Rejea changamoto iliyomkumba Stephane Aziz Ki kule Morocco akiwa na timu ya Taifa ya Burkina Faso
Alizuiwa kwa takribani siku nne nchini humo baada ya vipimo kuonyesha ana covid sambamba na wenzake wawili
Kama ingetokea Yanga kufanya vipimo vya covid Sudan na baadhi ya wachezaji kuonekana na maambukizi, sio tu wangekosa mchezo dhidi ya Al Hilal pengine wangekosa mchezo dhidi ya Simba kwani wangezuiwa nchini humo kwa siku kadhaa