Yanga ilivyokwepa hujuma Sudan

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Oct 2022
Yanga ilivyokwepa hujuma Sudan

Yanga itaondoka jijini Dar es salaam Jumamosi Oktoba 15 saa 10 Alfajiri na itawasili nchini Sudan Jumamosi hiyohiyo majira ya saa 5 asubuhi

Jioni ya siku hiyo Yanga itafanya mazoezi kwenye uwanja wa Al Hilal ambao utatumika siku ya Jumapili saa 2 usiku

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema kuondoka siku ya Jumamosi ni sehemu ya mkakati wao ili kupunguza muda ambao watakaa nchini Sudan

Mkakati huo utawasaidia kukwepa baadhi ya 'hujuma' ambazo hufanywa na wenyeji wao dhidi ya timu zinazokwenda kucheza Sudan

"Tumepunguza idadi ya siku za kukaa Sudan ili kupunguza hizo hujuma, tupo makini katika hii mechi, tuna wachezaji wazoefu ambao wanajua mazingira ya ugenini. Kilichotokea Dar ni sehemu ya matokeo, tumejipanga kupata ushindi ugenini na kutinga hatua ya makundi," alisema Injinia Hersi

Katika mchezo uliopita ambao Al Hilal walicheza na St George hapo Sudan, mashabiki wa timu hiyo waliwafanyia vurugu wachezaji wa St George wakiwa hotelini na baadae wakati timu inaelekea uwanjani

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeionya Al Hilal kudhibiti vurugu za mashabiki wao la sivyo wanaweza kudhibitiwa kuingiza mashabiki uwanjani

Msafara wa Yanga utakaoondoka Jumamosi utajumisha watu 51 ambapo wachezaji ni 25, benchi la ufundi 11, viongozi na mashabiki 15

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’