Yanga yatanguliza 'shushushu' Sudan

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Oct 2022
Yanga yatanguliza 'shushushu' Sudan

Yanga imedhamiria kwenda kusaka matokeo ya ushindi Sudan ili kuhakikisha inatinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Ili kuepuka hujuma za aina yoyote kutoka kwa wenyeji wao, tayari maafisa wa Yanga wametua Sudan kuweka mambo sawa

Uongozi wa Yanga unahakikisha kikosi kinakuwa katika mazingira bora kitakapokuwa Sudan kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa Jumapili Oktoba 16

Pamoja na kuwa Yanga iliwapa Al Hilal ukarimu wa hali ya juu walipokuja nchini, hakuna uhakika kama wenyeji wao nao watalipa ukarimu

Tayari kuna taarifa kuwa Al Hilal wamewagomea Azam TV kuonyesha mchezo huo 'mbashara' hivyo kuna uwezekano mchezo hautaonyeshwa na televisheni yoyote

Al Hilal walifanya hivyo kwenye mchezo wao dhidi ya St George ambao walishinda kwa bao 1-0, kupitia mkwaju wa penati ya Makabi Lilepo

Silaha kubwa ya Yanga kuelekea mchezo huo ni ubora wa kikosi na mbinu za Kocha Nasreddine Nabi

Yanga inatarajiwa kutoa nafasi kwa mashabiki ambao watapenda kuiunga mkono huko Sudan

Huenda Wananchi wakapaa na 'dege' la ATCL siku chache kabla ya mchezo na kurejea baada ya mchezo huo ili kuwahi maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
50m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’