Mwananchi kama huna tiketi hakikisha unaitumia vyema siku ya leo kukata tiketi yako ili uwe sehemu ya historia ambayo inakwenda kuandikwa uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya kesho Jumamosi
Ni mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Yanga dhidi ya Al Hilal, mchezo ambao Wananchi wanahitaji ushindi mnono ili kuwa katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi
Yanga imepania kumaliza mchezo hapahapa jijini Dar es salaam, wiki ijayo itakuwa siku ya kukamilisha hesabu kule Sudan
Mashabiki ni silaha muhimu sana kwa Yanga siku ya kesho, ndio maana Mwananchi kindakindaki hupaswi kubaki nyumbani
Jambo moja la uhakika ni kuwa wachezaji wa Yanga hawatawaangusha kwani wamejipanga na wana dhamira ya dhati ya kumaliza mechi hiyo kesho

ADVERTISE HERE