Moja ya sababu ambayo ilipelekea Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi kupendekeza winga mtukutu Bernard Morrison arejeshwe Yanga ni hii michuano ya Ligi ya Mabingwa
Hakuna mjadala Morrison alikuwa mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Simba ambacho msimu uliopita kilifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Watani wanaweza wasikubaliane na hili kwa sababu tu Morrison amerejea nyumbani lakini huo ndio ukweli, Morrison aliwasaidia sana kuwapa matokeo katika zile mechi muhimu
Ilikuwa habati mbaya kwa Morrison hakupata nafasi ya kucheza mechi za awali ligi ya mabingwa akiwa na Yanga kutokana na majeraha
Morrison sasa yuko fit kwa asilimia 100 na sasa Wananchi wanataka kuona anaifanya vyema kazi iliyomrejesha Yanga licha ya sintofahamu iliyojitokeza wakati alipotimkia Simba
Nabi ameweka imani kubwa kwa Morrison kuwa atashirikiana vyema na wenzake kuhakikisha Yanga inapata ushindi mnono siku ya Jumamosi
Morrison amepata muda wa kutosha kufanya mazoezi na wenzake na sasa hakuna wasiwasi Morrison yuko tayari