Timu ya Al Hilal inatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamisi wakitokea DR Congo, tayari kwa kuikabili Yanga kwenye mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya mabingwa Afrika utakaopigwa jumamosi tarehe 8 mwenzi huu
Baadhi ya maafisa wa timu hiyo tayari wamewasili nchini ambapo juzi walikuwepo dimba la Mkapa kushuhudia mchezo wa ligi kuu kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Yanga
Yanga ambao ni wenyeji wa mchezo huo, wanaendelea na maandalizi Avic Town habari njema ikiwa ni kurejea kwa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ambaye aliungana na wenzake jana
Yanga inahitaji kupata ushindi mnono katika mchezo huo wa kwanza ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi
ADVERTISE HERE