Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wameendeleza rekodi ya ushindi katika ligi kuu ya Vodacom baada ya kuilaza Majimaji mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Ushindi wa mchezo huo wa mzunguuko wa 18 unaifanya Yanga iwe imeshinda michezo mitano mfululizo tangu ilipotoka suluhu ya bila kufungana na Mwadui FC.
Iliwachukua dakika 19 tu Yanga kuandika bao la kuongoza kupitia mkwaju wa penati maridadi uliopigwa na Papi Tshishimbi.

Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi sambamba na kumtoa kwa kadi nyekundu mlinzi wa Majimaji Mpoki Mwakinyuke aliyezuia kwa mkono shuti la Obrey Chirwa lililokuwa linaelekea kimiani.
Ikiendelea kutawala mchezo huo Yanga iliandika bao la pili kwenye dakika ya 29 kupitia kwa kinara wake wa mabao Obrey Chirwa aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Gadiel Michael.
Nusura Buswita aiandikie Yanga bao la tatu kwenye dakika ya 39 baada ya shuti lake la chinichini kugonga mwamba kisha kuokolewa na walinzi wa Majimaji.
Katika dakika ya 43 Emanuel Martin akafunga moja ya mabao ya msimu baada ya kuachia fataki akiwa umbali wa karibu mita 25 na mpira kujaa kimiani.
Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili, licha ya kuwa pungufu Majimaji walirudi wakiwa na nguvu mpya na walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi kwenye dakika ya 56 kupitia mkwaju wa penalti uliofungwa na Marcel Kaheza baada ya beki Said Juma 'Makapu' kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Majimaji iliyotawala mchezo huku Yanga ikicheza kwa tahadhari kubwa kulinda mabao yake mawili.
Hata hivyo mabadiliko yaliyofanywa na kocha George Lwandamina kwa kuwaingia Juma Mahadhi na Geofrey Mwashiuya nafasi za Ibrahim Ajib na Pius Buswita yaliiongezea Yanga kasi ya mashambulizi.
Alikuwa ni nyota wa mchezo huo Papi Tshishimbi aliyefunga bao la nne kwa shuti kali kwenye dakika ya 81 baada ya kukutana na mpira uliokuwa umeokolewa na mabeki wa Majimaji nje kidogo ya 18.

Ushindi huo umeifanya Yanga ifikishe alama 37 ikiisogelea Simba iliyo kileleni na alama 41.
Simba itashuka kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga kesho kuumana na Mwadui FC.

ADVERTISE HERE