Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amerejea tayari kuungana na wenzake Avic Town katika maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Oktoba 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Aziz Ki alipata changamoto akiwa na timu ya Taifa ya Burkina Faso walipokwenda Morocco kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Comoros
Yeye na wenzake wawili walibainika kuwa na maambukizi ya covid hivyo kulazimika kubaki Morocco kulingangana na taratibu za nchi hiyo katika udhibiti wa Covid
Kuchelewa kwake kukapelekea akakosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting jana Wananchi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1

ADVERTISE HERE