Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki atawasili nchini Jumatatu baada ya kukumbana na changamoto nchini Morocco alikoenda na timu ya Taifa ya Burkina Faso kwa ajili ya mchezo wa kirafiki
Taarifa iliyotolewa na Yanga mapema leo, imebainisha kuwa Aziz Ki amebaki Morocco kutokana na taratibu za nchi hiyo kumlazimu baada ya kuwa mmoja wa wachezaji waliobainika na maambukizi ya Covid 19
Aziz Ki na wenzake wawili watafanyiwa vipimo vya awamu ya tatu leo na kama hatakuwa na maambukizi ataruhusiwa kuondoka na atawasili nchini Jumatatu
ADVERTISE HERE