Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amesema hakuna jambo muhimu kwake zaidi ya kuisaidia Yanga kufikia malengo yake hasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Yanga itacheza na Al Hilal Jumamosi ijayo kwenye mchezo wa kwanza kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo, Yanga ikianzia nyumbani
Malengo ya Yanga ni kutinga hatua ya makundi ili kumaliza ukame wa miaka 24 kukosa kushiriki hatua hiyo
Aziz Ki amesema anajivunia kuwa Yanga kwani ni klabu kubwa na anaamini itafanya vizuri mbele ya Al Hilal, licha ya kukiri ni timu ngumu
"Yanga iliniona kupitia michuano ya CAF nikiwa na Asec, nikiwa kule nilifanya nililoliweza na sasa nipo Yanga nitahakikisha nakuwa bora zaidi"
"Nataka kuendeleza rekodi kwa manufaa ya timu hii. Nina uzoefu, nitahakikisha sifanyi makosa pale nitakapopata nafasi, naamini kwa kushirikiana na wenzangu tutafanya vizuri," alisema Aziz Ki
Aziz Ki anatarajiwa kurejea Jumatatu kutokana na changamoto alizopata huko Burkina Faso