Tumejipanga kutinga makundi - Mtine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Sep 2022
Tumejipanga kutinga makundi - Mtine

Klabu ya Yanga kupitia Mtendaji Mkuu Andre Mtine amesema wana malengo makubwa msimu huu, kutwaa ubingwa wa ligi kuu na kufanya vizuri ligi ya mabingwa barani Afrika

Mtine amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanjani kuisapoti timu yao katika michezo hiyo muhimu

Amesema wanahitaji kupata matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani, shabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani

"Tunawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani, wingi wao ni muhimu sana na bila shaka tutaweza kufanya vizuri kwa umoja wetu"

"Pia nawatakia kila la kheri washiriki wengine Simba na Azam Fc kuelekea katika michezo yao kwani sote tunaiwakilisha Tanzania," alisema

Nae Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wamedhamiria kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Kamwe amesema hawatasikiliza maneno ya kuwakatisha tamaa kwa kuwa wako tayari kuisambaratisha Al Hilal

"Tumejipanga kufanya kitu cha tofauti ambacho hakijawahi kufanyika hapa Tanzania, tutaendelea kutoa taarifa mbalimbazli za utaratibu tutakaoutumia kuhakikisha tunaisambaratisha Al Hilal"

"Kwa wakati huu Yanga ni timu kubwa kuliko Al Hilal, tutalithibitisha hilo Oktoba 08. Mechi itachezwa saa 10 jioni uwanja wa Benjamin Mkapa"

"Viingilio Mzunguuko ni Tsh 3,000/- ambayo unapaswa kukata tiketi hii kabla ya mchezo, siku ya mchezo tiketi za Mzunguuko zitapatikana kwa Tsh 5,000"

"VIP B na C ni Tsh 10,000/- na VIP A ni Tsh 15,000/-, tumeweka viingilio rafiki kwa Wanachama na Mashabiki wetu waje kuiunga mkono timu yao"

"Tunawaomba Wanahabari watuunge mkono katika dhamira hii ya kulipigania Taifa. Msitoe taarifa zenye lengo ya kuwatisha na kuwakatisha tamaa mashabiki wetu wakati kiuhalisia Yanga ndio timu iliyokamilika zaidi miongoni mwa timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya CAF"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
43m ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’