Wakati Al Hilal wakitua DR Congo kabla ya kuja Tanzania kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Yanga, leo Ijumaa Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe atazungumza na wanahabari kuweka bayana mikakati kuelekea mchezo huo
Mkutano huo utafanyia Serena Hotel kuanzia saa nne asubuhi
Yanga imejipanga, ikiwa na dhamira ya kutumia vyema uwanja wa nyumbani kuhakikisha inaibuka na ushindi mnono katika mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 08
Matokeo mazuri kwa Yanga katika mchezo wa nyumbani, yatawaweka Wananchi katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi wakihitaji kutopoteza mchezo wa marudiano ambao utapigwa Oktoba 16 huko Sudan
Wapinzani wao Al Hilal wamewasili DR Congo kuweka kambi ya muda mfupi ambapo imeelezwa watacheza mechi za kirafiki dhidi ya TP Mazembe na AS Vita kabla ya kuja Tanzania
