Mlinzi wa kati wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' leo ameonekana akiitumikia klabu ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold ambapo Dodoma Jiji imeibuka na ushindi wa bao 1-0
Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa Ninja ametolewa kwa mkopo kuitumikia Dodoma Jiji mpaka mwisho wa msimu
Ikumbukwe Ninja aliongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga kwa mwaka mmoja zaidi
Lakini ni wazi amepelekwa Dodoma Jiji ili akapate nafasi ya kucheza na huenda akarejeshwa baada ya muda wake wa mkopo kumalizika
Kila la kheri kwake katika majukumu yake mapya...!
ADVERTISE HERE