Lwandamina aeleza umuhimu wa ushindi leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Feb 2018
Lwandamina aeleza umuhimu wa ushindi leo
Kocha wa Yanga, George Lwandamina, amesema moja ya sababu ya wapinzani wao wa leo, Majimaji ya Songea kukumbana na kipigo ni uchu wao wa kutaka kupunguza pengo la pointi lililopo kati yao na vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba.

Yanga leo inaikaribisha Majimaji kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku mabingwa hao watetezi wakiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Septemba mwaka jana mjini Songea.

"Mchezo utakuwa mgumu kama ilivyo michezo mingine, lakini haturidhishwi kuwa nyuma kwa pointi saba na wanaoongoza ligi (Simba), mchezo wa leo kwetu ni muhimu kushinda na pengo la pointi litatufanya tupambane kupata ushindi," alisema Lwandamina na kuongeza.

"Endapo tutateleza kesho (leo) na wapinzani wetu kushinda kwenye mchezo wao, itafanya kuwapo kwa tofauti ya pointi nyingi, wachezaji wangu wanafahamu umuhimu wa ushindi leo."

Katika hatua nyingine, Lwandamina amegundua upungufu kwenye safu yake ya ushambuliaji ambao wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi za kufunga na tayari ameanza kufanyia kazi kasoro hiyo.

"Tunajitahidi kutengeneza nafasi, lakini bado hatujawa makini kwenye umaliziaji, ni jambo tunaloendelea kulifanyia kazi," alisema Lwandamina.

Kwa upande wake kocha wa Majimaji, Habibu Kondo, amekiri mchezo wa leo kuwa mgumu, lakini wamejipanga kupambana na wapinzani wao.

Alisema wanaiheshimu Yanga kwa kuwa ni timu kubwa, lakini lolote linaweza kutokea ndani ya dakika 90 za mchezo.

Wakati Yanga wakiumana na Majimaji leo, Kesho kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, vinara wa ligi, Simba, watakuwa wageni wa Mwadui FC
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’