Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe leo kupitia redio mbalimbali ataweka bayana mikakati yake ya hamasa kuhakikisha Wananchi wanashiriki kikamilifu katika mechi muhimu zinazokuja
Oktoba 03 Yanga itachuana na Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu lakini Oktoba 08 Wananchi watakuwa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal
Kamwe amesema malengo ya Yanga msimu huu ni kuvuka hatua ya makundi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Yanga imedhamiria kufungua mnyororo uliowakwamisha kushiriki katika hatua hiyo kwa miaka 24 iliyopita
ADVERTISE HERE