Mfahamu CEO mpya wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Sep 2022
Mfahamu CEO mpya wa Yanga

Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine ana historia na CV kubwa inayomfanya kuwa chaguo sahihi kwa Yanga katika nafasi hiyo iliyoachwa na Senzo Mazingisa

Mtine raia wa Zambia anafahamika sana huko kwao (Zambia), amewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Nkana miaka ya 1980 na kuifanya iwe tishio Afrika kabla ya mwaka 2000-2004 alipotinga Power Dynamos ambayo ni klabu pinzani ya Nkana na kuifanya ishinde ubingwa wa Ligi Kuu ya Zambia na pia kubeba mataji matano ya ndani

Pia aliwahi kuitumikia kamati ya fedha ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kabla ya kutua TP Mazembe alikotumika kwa nafasi mbalimbali ikiwamo kuwa msaka vipaji 'skauti' wa klabu hiyo na kuipelekea timu hiyo nyota walioipa mafanikio makubwa barani Afrika na duniani ikiwamo kufika fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia 2010

Mtine pia ana taaluma ya usimamizi wa fedha ambapo aliwahi kuwa Mhasibu na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha soka Zambia (FAZ)

Mtine ni mtu wa mipango na taaluma yake ya kiuchumi na kujua soka kwa kiwango cha juu akirithi kipaji cha baba yake Tom Mtine aliyewahi kuwa Rais wa FAZ na mjumbe wa CAF

Yanga inaamini ni mtu sahihi kuchukua nafasi ya Senzo ambaye aliomba kupumzika baada ya kusimamia na kukamilisha mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’