Leo Yanga imemtangaza rasmi Mtendaji Mkuu wa klabu Mzambia Andrey Mtine ambaye anatua kuchukua nafasi iliyoachwa na Senzo Mazingisa
Mtine amepewa mkataba wa miaka miwili ambao utamfanya abaki Mitaa ya Twiga na Jangwani mpaka mwaka 2024
Wengi wana shauku ya kutangazwa kwa Afisa wa Habari zikiwa zimepita wiki kadhaa tangu Hassan Bumbuli amalize mkataba
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema kuanzia leo jioni Yanga itatangaza kikosi kazi cha vijana ambao watakwenda kufanya kazi katika Idara ya Habari na Digital kiujumla
"Leo jioni tutaanza kutangaza timu ya vijana watakaokuwa wanafanya kazi kwenye idara ya Habari ya Yanga," alisema Hersi
ADVERTISE HERE