TFF yamfungia Nyosso mechi tano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
13 Feb 2018
TFF yamfungia Nyosso mechi tano
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchini (TFF) imemfungia beki wa Kagera Sugar Juma Nyoso kucheza mechi tano pamoja na faini ya Tsh. 1,000,000 (Milioni moja) kwa kosa la kumpiga shabiki baada ya mchezo wa VPL kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Afisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema Kamati ya Nidhamu ya TFF ilijadili shauri la Nyosso ambalo lilifikishwa kwenye kamati hiyo baada ya kupokea taarifa ya mchezo.

“Juma Nyoso alituhumiwa kumpiga shabiki baada ya kumalizika kwa mchezo kinyume na kanuni za ligi kuu zinazozungumzia mchezo wa kiungwana.”

“Kamati ilipitia ripoti ya kamishna wa mchezo ambayo imeeleza tukio la kupishana kwa Juma Nyoso na shabiki ambaye alikuwa amebeba vuvuzela na Juma Nyoso akaonekana kusimama na kuanza kumpiga shabiki yule kwa kutumia kiatu na baadaye akamuinamisha na kuanza kumpiga kwa kutumia goti.”

“Kamati ilimwita Nyoso kujitetea, kwa upande wake alikataa madai hayo ya kumpiga shabiki. Alisema alichofanya ilikuwa ni kumkunja tu shabiki huyo lakini hakumpiga.”

“Kamati imemtia hatiani Juma Nyoso kupitia kanuni za ligi kuu na katiba ya TFF lakini ilipokea taarifa za nyuma za Nyoso kwamba aliwahi kuadhibiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Kwa hiyo kamati imemfungia Nyoso mechi tano pamoja na faini ya shilingi 1,000,000 (milioni moja).”
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →