Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa Ligi ya Bodi ya Ligi inapaswa kufanya maamuzi yake ndani ya 72 baada ya mchezo husika lakini inavyoonekana sasa sivyo
Ukiangalia adhabu iliyotolewa kwa mchezaji Benard Morrison, ni siku 16 zimepita tangu mchezo husika, jambo hili linaleta ukakasi kwani haipaswi kuwa hivi
Hakuna anayepinga adhabu aliyopewa Morrison lakini hoja iko kwenye muda na mazingira ya adhabu hiyo
Katika mazingira yake ni rahisi mtu kudhani wakati mwingine Kamati hii inaweza kutumika kuwanufaisha wengine
Yaani mchezaji anaweza kufanya kosa kwenye mchezo mmoja, adhabu isitolewe wakati husika, akaja kuadhibiwa katika nyakati ambazo kuna mechi muhimu ambayo pengine timu yake inamuhitaji sana mchezaji huyo
Ndicho kilichotokea kwa Morrison kwani Yanga haitaweza kumtumia katika mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Oktoba 23
Lakini kama Kamati hii ingefanya kazi yake kwa usahihi, Morrison angemaliza adhabu yake mapema na angeweza kushiriki mchezo huo
Jambo hili linapaswa kusemwa na wahusika walifanyie kazi, leo inatokea kwa Yanga pengine siku nyingine itatokea kwa timu nyingine na kuondoa maana ya Kamati hii