Kiungo Thabani Kamusoko amekuwa akifanya mazoezi ya kuimarisha mwili wake baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miezi mitatu akiuguza majeraha.
Habari njema ni kwamba Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu amemuwashia 'taa ya kijani' kiungo huyo kuwa sasa amepona kabisa na anaweza kuitumikia Yanga.
Ni uamuzi wa benchi la ufundi uliobaki juu ya kuanza kumtumia kiungo huyo.
Wakati huo huo, uongozi wa Yanga umesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 18 dhidi ya Majimaji yamekamilika.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Yanga leo, wachezaji watatu pekee watakaukosa mchezo huo kutokana na majeruhi.
Wachezaji hao ni Donald Ngoma, Yohana Nkomola na Amissi Tambwe.
Hii inamaanisha kuwa kiungo Thabani Kamusoko ambaye mashabiki 'wamem-mis' baada ya kukosekana dimbani kwa muda mrefu huenda akawa kikosini kesho kama benchi la ufundi litampa nafasi.
Ni habari njema pia kwa kureja kikosini kwa mlinda lango Youthe Rostand, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Andrew Vicent na Pato Ngonyani.

ADVERTISE HERE