Nabi atenga siku 10 za maandalizi kuwakabili Al Hilal

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Sep 2022
Nabi atenga siku 10 za maandalizi kuwakabili Al Hilal

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi, amesema siku 10 zinamtosha kukiandaa kikosi chake kuhakikisha kinafanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan

Yanga baada ya kuitoa Zalan FC ya Sudan Kusini katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 9-0, raundi ya kwanza sasa itaanzia nyumbani dhidi ya Al Hilal iliyoitoa St. George ya Ethiopia kwa faida ya bao la ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa 2-2.

Al Hilala ilikubali kipigo cha mabao 2-1 ugenini kabla ya kushinda nyumbani kwa bao 1-0, hivyo kunufaika na bao la ugenini, wakati Yanga yenyewe ilishinda mchezo wa kwanza mabao 4-0 na kisha wa marudiano kuibuka na ushindi wa 5-0, shukran kwa straika wao hatari, Fiston Mayele aliyetupia mabao sita kwa kufunga hat-trick katika kila michezo yote miwili.

Tayari Yanga wameanza mazoezi ya utimamu wa mwili 'gym' pale Gymkhana jijini Dar es Salaam na leo wataanza mazoezi ya uwanjani kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaofuatiwa na mchezo dhidi ya Al Hilal

Nabi amesema kabla ya kuvaana na Ruvu Shooting, watakuwa wamefanya mazoezi magumu ambayo yatawapa majibu kuelekea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Alisema mazoezi ya gym yatawasaidia wachezaji wake kuongeza stamina na kuwapa uwezo wa kupambana kwa dakika zote 90, kufanyia kazi mapungufu aliyoyaona kwenye mechi zilizopo.

"Nimeandaa programu maalum kwa wachezaji wangu, matarajio yangu siku 10 kuanzia leo hadi siku ya mechi, wachezaji watakuwa imara, hasa safu ya ushambuliaji kuwa makini kwa nafasi wanazozipata katika mechi," alisema Nabi.

Alisema wachezaji wake hawajapata muunganiko mzuri hivyo anahakikisha anaendelea kutengeneza taratibu kikosi chake na kupata matokeo mazuri katika michezo iliyopo mbele yao ikiwamo dhidi ya Ihefu na Ruvu Shooting na kisha dhidi ya Al Hilal Oktoba 8, mwaka huu.

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’