Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limeongeza kiasi cha pesa kwa timu zitakazofanya vizuri kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika kuanzia msimu huu
Katika viwango vipya, bingwa wa ligi ya mabingwa atapata kitita cha USD 3.5 Milioni ambazo ni sawa na Tsh BILIONI 8.1 za Kitanzania
Hapo awali bingwa alikuwa akipokea kitita cha USD 2.5 Milioni ambazo ni sawa na Tsh BILIONI 5.8
Kwa timu zitazotinga hatua ya robo fainali zitavuna USD 8,00,000.0 sawa na Tsh Bilioni 1.8
Timu zitakazotinga nusu fainali zitavuna USD 1 Milioni ambazo ni sawa na Tsh Bilioni 2.2
Mshindi wa pili ataondoka na kitita cha USD 1,750,000 Mil sawa na Tsh Bilioni 4
ADVERTISE HERE