Afisa Habari Yanga ni suala la muda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Sep 2022
Afisa Habari Yanga ni suala la muda

Klabu ya Yanga inakamilisha mchakato wa kuajiri Afisa wa Habari ambaye atakabidhiwa mikoba iliyoachwa na Hassan Bumbuli aliyemaliza mkataba

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema kila kitu kinakwenda vizuri na kuwa watatangaza pale mchakato huo utakapokamilika

Aidha Arafat amesema Yanga inaendesha mchakato wa kujaza nafasi ya Afisa Habari kwa kufuata kanuni na taratibu walizojiwekea ikiwemo kukidhi matakwa ya kikatiba

"Yanga haiweza kupangiwa mtu wa kumuajiri hivyo Wananchi wafahamu mchakato unaendelea vizuri na karibuni tutatangaza," alisema

Hivi karibuni kumeibuka marumbano kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya wachambuzi wakimtuhumu aliyekuwa Msemaji wa Yanga Haji Manara kukwamisha kuajiriwa kwa moja ya wachambuzi mwenzao(Jina kapuni)

Hata hivyo Manara aliwajibu wachambuzi hao akihoji imekuwaje wakati huu wanapigia debe nafasi hiyo wakati mwanzoni walikuwa wakiponda utaratibu wa klabu kuwa na wasemaji wakitolea mfano huko Ulaya timu hazina wasemaji

Manara amesema yeye hahusiki na mchakato huo kwa kuwa amefungiwa miaka miwili na TFF ingawa bado ni mwajiriwa wa Yanga

"Yanga haiwezi kupangiwa imuajiri nani, itaajiri kwa kufuata taratibu na utamaduni wa klabu yetu," alisema Manara

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’