Baada ya Yanga kuvuka hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa kwa kuifumua Zalan Fc kwa ushindi wa jumla wa mabao 9-0 katika michezo yote miwili, sasa itakutana na Al Hilal ya Sudan ambayo iliiondosha St George kwa faida ya bao la ugenini baada ya matokeo ya sare ya mabao 2-2
Habari njema kwa Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Al Hilal ni uwezekano wa kumtumia winga Tuisila Kisinda
Yanga tayari imepokea leseni ya Kisinda kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) ambayo inamruhusu kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa
Kabla ya kuivaa Al Hilal, Kisinda ataanza kuuwasha moto kwenye ligi wiki ijayo katika michezo dhidi ya Ihefu Fc na Ruvu Shooting


ADVERTISE HERE