Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga watakutana na Al Hilal ya Sudan kwenye mchezo wa raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Al Hilal wamepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya St George huko Sudan hivyo kutinga raundi ya kwanza kwa faida ya bao la ugenini
St George walipata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Ethiopia
Mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa jijini Dar es salaam kati ya Oktoba 7-9 na marudiano kupigwa huko Sudan Oktoba 14-16
Hii ni raundi ya mwisho kuelekea hatua ya makundi
ADVERTISE HERE