Bila shaka winga Bernard Morrison atakuwepo dimbani siku ya Jumamosi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa, mkondo wa pili dhidi ya Zalan Fc
Yanga inakwenda kukamilisha dakika 90 za awamu ya pili ikiwa na mtaji wa mabao manne baada ya ushindi wa 4-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza
Morrison hakuwa sehemu ya mchezo wa kwanza baada ya kupata majeraha katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc uliopigwa Septemba 06 na kumalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
Morrison anajifua na wachezaji wenzake na bila shaka kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alimpumzisha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ili aimarike zaidi tayari kuwakabili Zalan Fc
Pamoja na mtaji wa mabao manne, wachezaji wa Yanga 'wanautaka' kwelikweli mchezo wa Jumamosi
Pengine wanataka kutuma ujumbe kwa timu nyingine zinazoshiriki ligi ya mabingwa kuwa msimu huu Wananchi wana jambo lao katika michuano hiyo