Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Simon Patrick amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar
Simon amesema kwa ubora walionao Mtibwa Sugar msimu huu, anatarajia mchezo mkali wenye hadhi ya ligi kuu
"Tunatarajia mechi itakuwa ngumu na yenye ushindani wenye hadhi ya Ligi kuu. Niwaombe Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye dimba la Benjamin Mkapa kuweza kuwapa hamasa na nguvu Wachezaji wetu," alisema Simon
Mtibwa Sugar wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama saba na kufunga mabao saba huku wakiruhusu mabao manne
Yanga inashika nafasi ya tatu pia ikiwa na alama saba lakini imefunga mabao sita na kuruhusu mabao matatu
Simba inaongoza ligi ikiwa na alama saba wakifunga mabao saba na kuruhusu mabao mawili
Namungo Fc na Singida Big Stars zinashika nafasi ya nne na tano pia zikiwa na alama saba
Ushindi kwa Yanga leo utawapeleka kileleni mwa msimamo wa ligi