Baada ya ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Zalan Fc katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga inahamishia nguvu kwenye ligi ambapo siku ya Jumanne itakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuumana na Mtibwa Sugar
Mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali, utapigwa kuanzia saa moja usiku
Mtibwa Sugar wameanza vyema msimu huu wakishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama saba sawa na Yanga lakini wao wamefunga mabao mengi zaidi
Utakuwa mchezo wa pili kwa Yanga kucheza nyumbani msimu huu, ukiwa ni mchezo wa raundi ya nne
ADVERTISE HERE