Tuwape heshima wachezaji wetu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Sep 2022
Tuwape heshima wachezaji wetu

Ni bahati mbaya wakati mwingine mashabiki tunaingia kwenye mkumbo wa vitu ambavyo malengo yake hatuyafahamu

Huko kwenye 'maredio' wachambuzi huanzisha mijadala ya kuwashusha thamani baadhi ya wachezaji wa Yanga

Siku za karibuni amelengwa zaidi nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, bahati mbaya nasi tumeungana nao kuimba nyimbo ambazo hatufahamu malengo yake

Utasikia Mwamnyeto amechoka, ameshuka kiwango, Mwamnyeto sijui hataisaidia Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

Nafikiri kwa sasa ukizungumzia walinzi bora wa kati ndani ya nchi basi utamtaja Mwamnyeto na Dickson Job

Awali walianza na Job wengine wakimhukumu kwa umbile lake lakini kazi yake nzuri uwanjani ikawanyamazisha na sasa wamehamia kwa Mwamnyeto

Katika misimu mitatu mfululizo Mwamnyeto amekuwa mchezaji wa timu ya Taifa na ametumika katika vikosi vya makocha mbalimbali

Yanga inakwenda kucheza ligi ya mabingwa inahitaji wachezaji wenye uzoefu wa mechi za Kimataifa, Mwamnyeto ni mmoja wao

Sio kila mechi mchezaji anaweza kucheza katika ubora uleule lakini kinachoangaliwa zaidi ni ule mchango wake wa jumla kwenye mafanikio ya timu

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi hukerwa na maswali ya wanahabari wanaohoji kwa nini timu yake inaruhusu mabao licha ya kuwa hakuna mechi ambayo Yanga imepoteza

Hakuna kocha ambaye anafurahi timu yake iruhusu mabao lakini muhimu ni yale matokeo ya jumla yanayopatikana baada ya dakika 90

Yanga hii imecheza mechi 40 za ligi pasipo kupoteza, Mwamnyeto ni sehemu ya mafanikio hayo

Msimu uliopita pengine Mwamnyeto ndiye mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi kwenye kikosi cha Yanga

Msimu huu ana bao moja katika mabao sita yaliyofungwa na Yanga kwenye ligi

Huyu ni mchezaji ambaye mchango wake kwenye kikosi cha Yanga hauna mashaka nadhani anastahili heshima

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’