Maswali yamekuwa mengi kwa kiwango cha mlinda lango namba moja wa Yanga Djigui Diarra ambaye msimu huu tayari ameruhusu mabao matatu katika mechi mbili za ligi alizocheza
Tangu mchezo wa fainali kombe la FA msimu uliopita dhidi ya Coastal Union, Diarra ameruhusu bao katika kila mchezo aliocheza
Yapo mabao ambao ambayo mlinda lango huyo hawezi kulaumiwa lakini yapo pia ambayo anaweza kupewa lawama
Zipo nyakati ngumu ambazo mchezaji yeyote anaweza kupita, lakini nyakati hizo hazidumu
Ni wazi Diarra hafurahishwi na mwenendo wake wa kuruhusu mabao katika mechi alizotumika msimu huu
Wananchi hawapaswi kuwa na shaka na mlinda lango huyo bora wa ligi kuu msimu uliopita akimaliza na 'cleensheet' 16
Kama kuna changamoto za kiufundi zinamkabili, kocha wa makipa Milton Neinov ni jukumu lake kuhakikisha anamuimarisha ili kuwarudishia Wananchi 'mdaka mishare' wao waliomzoea