Tuko tayari kuikabili Azam Fc - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Sep 2022
Tuko tayari kuikabili Azam Fc - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kuelekea mchezo huo, Nabi amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo ambao wamedhamiria kushinda

"Tumepata muda mzuri wa kufanya mazoezi pamoja wakati wa mapumziko wa mechi za Kimataifa. Tulikuwa na muda mfupi wa pre-season hivyo wakati huu tumeutumia vizuri kujiimarisha"

"Nafurahi wachezaji wameonyesha utayari kuelekea mchezo dhidi ya Azam. Nimepata nafasi ya kuwaangalia Azam Fc katika michezo yao, nafikiri utakuwa mchezo mzuri na wenye ushindani," alisema Nabi

Akizungumzia afya za wachezaji wake, Nabi amesema Djuma Shabani alikuwa akisumbuliwa na maralia lakini alianza mazoezi jana pia mlinda lango Djigui Diarra ambaye alikuwa majeruhi nae ameanza mazoezi

"Tutawaangalia kwenye mazoezi ya mwisho leo, kuona kama tutaweza kuwatumia hapo kesho"

Nabi pia amebainisha wachezaji waliokuwa na majukumu ya timu ya Taifa nao watafanya mazoezi ya mwisho na wenzao leo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’