Mjadala wa hatma ya winga Tuisila Kisinda kuitumikia Yanga tuwaachie wanasheria watafute mwafaka huko TFF
Kwa upana wa kikosi cha Yanga nafikiri Wananchi hatuna sababu ya kupoteza muda wetu katika suala hili
Kama haiwezekani Kisinda kuitumikia Yanga wakati huu na Yanga imekamilisha usajili wake, dirisha dogo sio mbali, atasasajiliwa tu
Yanga inakabiliwa na mchezo muhimu wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc hapo kesho, Yanga inawahitaji mashabiki wake kwa wingi dimba la Mkapa katika mchezo huo
Mjadala huu ni kama unafifisha hamasa kuelekea mchezo huo muhimu ambao Yanga inazihitaji alama zote tatu
Hili lisitutoe 'kwenye reli', mwezi huu Yanga inacheza mechi tano, tatu za ligi kuu na mbili za ligi ya mabingwa
Ni mwendo wa kukusanya alama tatu kwenye kila mchezo wa ligi kuu na kufuzu raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa katika mchezo dhidi ya Zalan Fc, mchezo wa kwanza ukipigwa uwanja wa Azam Complex, Jumamosi Septemba 10