Kocha Msaidizi wa Yanga Cedrick Kaze amesema kurejea kwa winga Tuisila Kisinda kutakuwa na manufaa makubwa kwa timu hiyo katika mashindano ya ndani na ligi ya mabingwa
Kisinda amerejea Yanga akitokea klabu ya RS Berkane aliyoitumikia msimu uliopita, akiwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika
Kaze amesema Kisinda atawasili nchini wakati wowote kujiunga na wenzake wanaoendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Septemba 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
"Kisinda ni mchezaji mzuri nina imani ataendeleza ushindani wake kwenye ligi na mechi za Kimataifa"
"Tulikuwa na changamoto ya washambuliaji wa pembeni, kumpata Kisinda ni faraja kubwa kwetu kwani atatuongezea nguvu katika eneo hilo ndio maana tukaamua kumrudisha nyumbani," alisema Kaze
Saad Kawemba ambaye ni Mkurugenzi wa Mashindano katika klabu ya Yanga amesema Kisinda amerejeshwa baada ya mapendekezo ya benchi la ufundi na anaamini atakidhi matarajio ya klabu hiyo