Saa 5:59 usiku wa kuamkia leo Yanga ilifunga dirisha la usajili kwa kumtambulisha winga Tuisila Kisinda aliyerejea kwa Wananchi akitokea klabu ya RS Berkane
Kisinda anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Yanga katika dirisha hili la usajili ambalo limefungwa rasmi
Wachezaji wengine waliosajiliwa katika dirisha hili ni Stephane Aziz Ki, Lazarus Kambole, Gael Bigirimana, Bernard Morrison na Joyce Lomalisa
Idadi ya nyota wa kigeni kwenye kikosi cha Yanga sasa ni 14 ukimjumuisha na Yacouba Songne ambaye ameendelea kubaki kikosini na pengine atashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa tu
Ujio wa Kisinda unamaanisha kuwa Yanga pia imelazimika kuondoa jina la nyota mmoja wa kigeni kwenye usajili wa ndani ili Kisinda achukue nafasi yake
Yanga inatarajiwa kutoa taarifa ya kikosi chake kwa ajili ya michuano ya ndani na ile ya ligi ya mabingwa