Chirwa ajipe likizo kupiga penati

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Feb 2018
Chirwa ajipe likizo kupiga penati
Moja ya sifa kubwa ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa ni upambanaji wake awapo dimbani. Aina yake ya uchezaji imekuwa ikiinufaisha sana Yanga.

Katika mchezo wa leo dhidi ya St Louis Chirwa alikosa mkwaju wa penati wakati ambapo Yanga ilikuwa 'on-fire' ikisaka bao la kuongoza.

Kama Chirwa angefunga penati ile iliyotolewa kwenye dakika ya 25 pengine ingewafanya St Louis wafunguke na kuipa nafasi Yanga kupenyeza mipira zaidi langoni.

Kukosa penati sio jambo geni, na sio kosa lakini linaweza kumuathiri mpigaji kama atakuwa akikosa mara kwa mara.

Baada ya kukosa mkwaju wa penati kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi dhidi ya URA visiwani Zanzibar, Chirwa alikuwa na shauku ya kusahihisha makosa yake.

Aliipata nafasi kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Ihefu FC akafanikiwa kufunga penati kwenye dakika za majeruhi na kuirudisha Yanga mchezoni.

Lakini akaja kukosa tena kwenye changamoto ya mikwaju ya penati baada ya matokeo ya 1-1 dhidi ya Ihefu FC.

Akachukua majukumu kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji, akafunga.

Leo tena akabeba jukumu kwa kuwa anaamini yeye ni miongoni mwa wapiga penati wazuri, bahati mbaya amekosa.

Kwa kiasi fulani tukio la kukosa penati lilimuathiri na kumtoa mchezoni.

Nadhani itakuwa busara kama Chirwa atajipa (atapewa) likizo ya kupiga mikwaju ya penati kwa muda kwani mwenendo wake wa kosa-funga-kosa unamuweka kwenye wakati mgumu.

Yanga inao wachezaji wengi wanaoweza kumsaidia Chirwa kupiga mikwaju ya penati japo kwa muda.

Raphael Daudi Lothi, Hassani Kessy, Kelvin Yondani na hata Gadiel Michael ni wapigaji penati wazuri tu.

Wakati mwingine hebu benchi la ufundi liwajaribu hawa, kumpunguzia mzigo Chirwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’