Morrison apewa mazoezi maalum

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Aug 2022
Morrison apewa mazoezi maalum

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ndiye aliyependekeza usajili wa winga Bernard Morrison kutoka klabu ya Simba

Ni usajili ambao mashabiki wengi wa Yanga hawakuutarajia, kutokana na sintofahamu iliyotokea kati yake na Yanga pale alipoamua kuukana mkataba halali aliosaini Yanga na akajiunga na Simba

Morrison hakuhitaji muda mrefu kuonyesha thamani yake baada ya kurejea Yanga kwani katika michezo miwili ya ligi msimu huu amefunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao

Hata hivyo Nabi amebainisha kuwa Morrison bado hajafikia katika ubora anaouhitaji hivyo amemuandalia program maalum ya mazoezi

Nabi amesema Morrison akiwa katika ubora atakuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga hasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

"Kulingana na ubora wa kikosi changu, nimeona nimpe Morrison mazoezi mengine tofauti ili kuwa imara zaidi na tayari kwa asilimia zote kwa sababu nina imani kubwa ya kufanya vizuri dhidi ya Zalan FC ili nitinge hatua inayofuata," alisema Nabi.

Morrison anasimamiwa mazoezi na prof Healmy Gueldich ambaye anahakikisha raia huyo wa Ghana anakuwa 'fit' sawasawa

"Tunahitaji kuwa na mawinga walio tayari kiushindani kabla ya kuingia katika hatua ya pili ya mtoano, Morrison bado hajawa katika kiwango bora ambacho tunakitaka, ndio maana tunamjenga zaidi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’