Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo amesema Bodi yake haihusiki na mchezo wa Ngao ya Jamii
Kasongo amebainisha hayo kujibu maswali ya wadau wa soka wanaohoji kwa nini tukio la rafu aliyofanya mlinzi wa Simba Hennock Inonga dhidi ya kiungo wa Yanga Salum Abubakar 'Sure Boy' hakuna adhabu iliyochukuliwa
Kasongo amesema mchezo wa Ngao ya Jamii unasimamiwa na Kamati ya Mashindano ya TFF na sio Bodi ya Ligi
"Mchezo wa Ngao ya jamii unasimamiwa na kamati ya mashindano ya (TFF) na sio Bodi ya ligi, Kuhusu tukio la Inonga kwa Sure boy hilo ni la kamati ya mashindano ya (TFF), Waulizwe kamati ya Mashindano," Kasongo aliiambia Clouds fm
ADVERTISE HERE