FT : Yanga 1-0 St Louis

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Feb 2018
FT : Yanga 1-0 St Louis
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga leo wameanza vyema michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kuichapa St Louis bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa.

Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi kusaka bao la mapema lakini kukosekana umakini katika lango la St Louis kuliinyima Yanga ushindi mnono.

Mfumo uliotumiwa na klabu ya St Louis ulikuwa wa kujilinda zaidi 'kupaki basi' wakitafuta matokeo ya sare ugenini.

Yanga ingeweza kuandika bao la kuongoza kwenye dakika ya 25 baada ya Hassani Kessy kuangushwa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kutoa mkwaju wa penati.

Obrey Chirwa alikosa penati hiyo.

Karibu kipindi chote cha kwanza Yanga iliishambulia St Louis iliyokuwa imejaza wachezaji wote langoni kwake kujilinda.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Juma Mahadhi aliyeingia kwenye dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib ambaye hakuwa katika ubora wake uliozoeleka pengine ni kutokana na majeruhi yaliyomuweka nje kwa takribani wiki mbili.

Kwa kiasi kikubwa mfumo wa kujilinda uliotumiwa na St Louis umeweza kuwasaidia wasifungwe mabao mengi hivyo kuufanya mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo kuwa mgumu kwa Yanga.

Hata hivyo matokeo ya ushindi ni muhimu zaidi kwa Yanga kwani sasa itawalazimu St Louis kushinda kwenye mchezo huo wa marudio.

Hali hiyo itafanya mchezo huo uwe wazi na Yanga itakuwa na nafasi ya kufunga mabao ugenini na kuweza kusonga mbele kutokana na ubora wake ukilinganisha na wapinzani wao wanaocheza soka la kawaida.

Aidha winga Juma Mahadhi ameendelea kudhihirisha kuimarika kwa kiwango chake kwani amekuwa akifanya vizuri kila anapopewa nafasi na benchi la Ufundi.

Kuingia kwake sambamba na Geofrey Mwashiuya kuliongeza kasi ya mashamulizi ya Yanga kupelekea kupatikana kwa bao hilo pekee.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’