Kwa wale wanaohoji kuhusu mshambuliaji Lazarus Kambole, watulie kwani nyota huyo kutoka Zambia ameanza kukiwasha Avic Town
Kambole ameanza mazoezi na wachezaji wenzake baada ya kupona majeraha ya misuli yaliyomfanya akosekane katika michezo ya mwanzo ukiwemo ule wa utambulisho wa wachezaji, wiki ya Mwananchi
Kambole amemuongezea kocha Nasreddine Nabi machaguo katika safu yake ya ushambuliaji kwani nyota huyo anaweza kutumika kama mshambuliaji wa kati au winga
Katika mazoezi yanayoendelea Avic Town, Nabi amekuwa akimtumia katika nafasi ya ushambuliaji wa kati zaidi
Nabi hataki kikosi chake kimtegemee mshambuliaji mmoja tu (Mayele) ndio maana msimu huu kwenye baadhi ya mechi alimuanzisha Makambo, bila shaka Kambole nae atatumika katika utaratibu huo
Yanga inaendelea na mazoezi makali Avic Town kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Septemba 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa