Huyo Moloko amezaliwa upya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Aug 2022
Huyo Moloko amezaliwa upya

Kabla ya msimu huu kuanza tetesi zilikuwa nyingi kumuhusu winga Jesus Moloko kuwa pengine angetolewa kwa mkopo

Hata hivyo dakika 45 za mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba zilitosha kuwakumbusha Wananchi yule Moloko aliyesajiliwa msimu uliopita

Moloko ni kama amepindua meza akiwa tayari ametoa pasi moja ya bao lililofungwa na Bernard Morrison katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

Katika mchezo huo Moloko alipata majeraha na kuwapa hofu Wananchi kuwa pengine angekaa nje kwa muda mrefu

Habari njema ni kuwa Moloko tayari amerejea uwanjani akiendelea na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Septemba 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Ni huyu huyu Moloko aliyewaliza Azam fc msimu uliopita akifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 2-0 kwa Yanga

Alipiga bao la 'kideoni' ambalo kabla Yanga wlaipiga pasi takribani 22. Septemba 06 Azam wanaye tena!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’