Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kesho Jumapili inaendelea na kampeni zake za kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) itakapoikaribisha Uganda Cranes kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Hii ni hatua ya pili kwa Taifa Stars katika mbio za kusaka kufuzu kwa fainali za Chan 2023 zitakazofanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi Februari 5 2023
Katika hatua ya kwanza, Tanzania ilifanikiwa kuiondoa Somalia na kupata nafasi ya kucheza dhidi ya Uganda ili kupata timu itakayokwenda Algeria katika fainali hizo.
Kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha Kim Poulsen kiko kambini kwa siku kadhaa kikijiandaa kwa mchezo dhidi ya The Cranes utakaofanyika kesho Jumapili kwa Mkapa
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni